Pata taarifa kuu
SOKA-FIFA

FIFA yaagiza mechi kati ya Senegal na Afrika Kusini kurudiwa

Nembo ya Shirikisho la soka duniani FIFA
Nembo ya Shirikisho la soka duniani FIFA REUTERS/Arnd Wiegmann/Files

Shirikisho la soka duniani Fifa limeagiza kuchezwa upya kwa mchezo wa kufuzu kombe la dunia nchini Urusi kati ya Afrika Kusini na Senegal baada ya mwamuzi aliyechezesha mchezo huo kufungiwa maisha na shirikisho hilo.

Matangazo ya kibiashara

Mwamuzi Joseph Lamptey raia wa Ghana amefungiwa kutojihusisha na masuala ya soka maisha yake yote baada ya kukutwa na hatia ya kupanga matokeo.

Mwamuzi huyu aliizawadia Afrika Kusini adhabu ya penati katika mchezo iliyopata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Senegal mwezi Novemba mwaka jana kwa kile muamuzi alidai ni mchezaji wa Senegal Kalidou Koulibaly aliushika mpira kwenye eneo la hatari wakati ulimgonga kwenye goti.

Mchezo huu wa marudiano umepangwa kufanyika mwezi Novemba mwaka huu wakati wa dirisha la kimataifa.

Lamptey alikuwa amefungiwa maisha mwezi Machi mwaka huu lakini Jumatano ya wiki hii mahakama ya kimataifa ya michezo CAS iliunga mkono adhabu hiyo.

Kwenye msimamo wa sasa kwenye kundi lao timu ya Senegal na Afrika Kusini zinashikilia nafasi ya tatu na ya nne kwenye kundi D nyuma ya Burkina Faso na Cape Verde.

Ni timu ambazo zitakuwa kileleni katika kila kundi ndizo zitakazofuzu kucheza fainali za kombe la dunia mwakani nchini Urusi.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.