Pata taarifa kuu
SOKA-MICHEZO

Rooney akabiliwa na kosa la kuendesha gari akiwa mlevi

Nahodha wa timu ya taifa ya Uingereza, Wayne Rooney akiwapa ishara ya dole mashabiki wa timu yake ya taifa wakati wa mchezo dhidi ya Malta ambapo aliiongoza kuibuka na ushindi wa mabao 2-0, 8 October 2016.
Nahodha wa timu ya taifa ya Uingereza, Wayne Rooney akiwapa ishara ya dole mashabiki wa timu yake ya taifa wakati wa mchezo dhidi ya Malta ambapo aliiongoza kuibuka na ushindi wa mabao 2-0, 8 October 2016. Reuters / Stefan Wermuth Livepic

Wayne Rooney, nahodha wa zamani wa kikosi ya ingereza cha Manchester United, anatatajiwa kuripoti mahakamani leo Jumatatu baada ya kushtumiwa kuendesha gari akiwa mlevi.

Matangazo ya kibiashara

Nyota huyo natarajiwa kufika mahakamani katika mji wa Stockport siku moja baada ya kurejea Old Trafford kwa mara ya kwanza tangu ajiunge na Everton.

Bw. Rooney alikamatwa wakati polisi walisimamisha gari lake katika eneo la Wilmslow, jijini Cheshire Septemba mosi.

Hata hivyo Wayne Rooney mwenye umri wa miaka 31, mzaliwa wa Liverpool, aliachiliwa kwa dhamana baada ya kushtakiwa kwa kuendesha gari akiwa mlevi.

Wayne Rooney, baba wa watoto watatu anashikilia rekodi ya kufunga mabao mengi zaidi nchini Uingereza.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.