Pata taarifa kuu
SOKA-CAF

Klabu bingwa / Shirikisho: TP Mazembe yafuzu nusu fainali kwa ushindi mkubwa

Wachezaji wa TP Mazembe wakisherehekea
Wachezaji wa TP Mazembe wakisherehekea www.tpmazembe.com

TP Mazembe, mabingwa watetezi wa taji la Shirikisho barani Afrika, watamenyana na FUS Rabat ya Morocco katika hatua ya nusu fainali.

Matangazo ya kibiashara

Mechi hiyo itachezwa mwishoni mwa mwezi huu, nyumbani na ugenini kabla ya kufika katika hatua ya fainali.

Mazembe ikicheza nyumbani katika uwanja wa Kamalondo mjini Lubumbashi, kwa jumla ya mabo 7-1 dhidi ya Al-Hilal Al-Ubayyid ya Sudan.

Mchuano wa kwanza, Mazembe waliwashinda wapinzani wao kwa mabao 2-1 na baadaye kuwalemea nyumbani kwa mabao 5-0.

FUS Rabat nao walifuzu baada ya kuishinda CS Sfaxien kwa mabao 5-4 baada ya sare ya bao 1-1 baada ya mechi zote mbili za nyumbani na ugenini.

SuperSport United ya Afrika Kusini nayo itamenyana na Club Africain ya Tunisia.

Club Africain ilifuzu baada ya kuishinda MC Alger mwa mabao 2-1, huku ZESCO United ikiondolewa baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 na Supersport United ambayo ilipata bao la ugenini.

Ratiba ya nusu fainali michuano ya klabu bingwa:-

  • Etoile du Sahel vs Al-Ahly
  • USM Alger vs Wydad Casablanca

 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.