Pata taarifa kuu
SOKA-LA LIGA

Barcelona yailemea Real Madrid 3-0 Santiago Bernabeu

Lionel Messi na  Luis Suarez wakisherehekea ushindi dhidi ya Real Madrid
Lionel Messi na Luis Suarez wakisherehekea ushindi dhidi ya Real Madrid REUTERS/Sergio Perez

Barcelona imepata ushindi mkubwa wa mabao 3-0 dhidi ya Real Madrid ugenini katika mchuano muhimu wa kuwania ligi kuu ya soka nchini Uhispania.

Matangazo ya kibiashara

Real Madrid walilemewa nyumbani katika uwanja wao wa  Santiago Bernabeu na kuruhusu mabao ya Luis Suarez, Lionel Messi na Aleix Vidal kuwaacha wakiwa na huzuni.

Matokeo haya yameonekana kama ya kulipiza kisasi baada ya kufungwa na wapinzani wao mabao 5-1 mwezi Agosti.

Ushindi huu wa Barcelona, unaiweka alama 14 mbele ya Real Madrid katika harakati za kutafuta ubingwa msimu huu.

Barcelona inaongoza rekodi ya kutofungwa na Real Madrid katika michuano 25 ilizocheza katika miaka ya hivi karibuni.

Barcelona inaongoza msimamo wa ligi kwa alama 45, huku Real Madrid ikiwa katika nafasi ya nne kwa alama 31.

Nafasi ya pili inashikiliwa na Atletico Madrid kwa alama 36, hiku Valencia ikiwa nafasi ya tatu kwa alama 34.

 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.