Pata taarifa kuu
CHAN-UGANDA

Kikosi cha Uganda Cranes kuelekea michuano ya CHAN 2018 chatajwa

Kikosi cha timu ya taifa, Uganda Cranes
Kikosi cha timu ya taifa, Uganda Cranes www.fufa.co.ug

Wachezaji 30 wa timu ya taifa ya soka ya Uganda, wametajwa kuanza maandalizi ya fainali ya kuwania taji la ska barani Afrika kwa wachezaji wanaocheza soka nyumbani CHAN 2018.

Matangazo ya kibiashara

Kikosi hicho kitapunguzwa na kufikia wachezaji 23, kuelekea michuano hiyo itakayofanyika nchini Morocco kati ya mwezi Januari na Februari.

Uganda Cranes inaanza mazoezi siku ya Jumatano katika uwanja wa Namboole jijini Kampala.

Wapenzi wa soka nchini Uganda wanasubiri kutajwa kwa kocha mpya tarehe 31 mwezi Desemba.

Makocha wanaotafuta nafasi hiyo ni pamoja na Mganda Moses Basena, Mfaransa Sebastien Desabre, Johnny McKinstry kutoka Ireland Kaskazini na Emilio Ferrera kutoka Ubelgiji.

Wachezaji walioitwa kambini:-

Makipa: Watenga Isma (Vipers Sc), Ochan Benjamin (KCCA FC), Ikara Tom (J-Kirinya SS), Saidi Keni (Proline FC)

Wadada Nicholas (Vipers Sc), Nsubuga Joseph (Sc Villa Jogoo), Muleme Isaac (KCCA FC), Madoi Aggrey (Police FC), Awanyi Timothy (KCCA FC), Muwanga Bernard (Sc Villa Jogoo), Bakaki Shafiq (Vipers SC), Lwanga Taddeo (Vipers SC).

Masiko Tom (Vipers SC), Saddam Juma (KCCA FC), Mutyaba Muzamiru (KCCA FC), Karisa Milton (Vipers SC), Mucureezi Paul (KCCA FC), Kateregga Allan (KCCA FC), Kyambadde Allan (SC Villa Jogoo), Nsibambi Derrick (KCCA FC), Shaban Muhammad (KCCA FC).

Senkatuka Nelson (Bright Stars FC), Kaweesa Hood (Police FC), Isiagi Daniel (Proline FC), Mujuzi Mustapha ( Proline FC), Kasule Abubaker (Express FC), Kagimu Shafik (URA FC), Kasozi Nicholas (Sc Villa Jogoo), Ahebwa Brian (Mbarara City FC), Kiiza Mustapha (KCCA FC).

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.