Pata taarifa kuu
LIVERPOOL

Mohamed Salah atamani kuisaidia Liverpool kushinda ligi kuu

Mshambuliaji wa Misri na klabu ya Liverpool Mohamed Salah.
Mshambuliaji wa Misri na klabu ya Liverpool Mohamed Salah. Phil Noble/Reuters

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Misri Mohamed Salah amesema ana matumaini kuwa anaweza kuisadia Liverpool kushinda ligi kuu ya soka nchini Uingereza msimu huu.

Matangazo ya kibiashara

Liverpool ambayo ina alama 35 katika nafasi ya nne, inacheza na Swansea City siku ya Jumanne katika mchuano muhimu wa ligi kuu.

Klabu hiyo yenye makao yake Anfield, ilinyakua taji hili mara ya mwisho mwaka 1990.

Hata hivyo, mwaka 2012 ilishinda taji la kombe la FA.

Salah raia Misri mwenye umri wa miaka 25 anayevalia jezi namba 11, aliungana na Liverpool akitokea klabu ya Roma nchini Italia na ameifungia klabu yake mabao 21.

“Ningependa kushinda maji nikiwa hapa, nilikuja hapa kushinda mataji,” amesema Salah.

Mchezaji huyo yupo katika orodha ya wachezaji watatu wanaowania taji la mchezaji bora barani Afrika mwaka 2017.

Mbali na Liverpool, Salah amewahi kuichezea Basel FC, Chelsea, na Fiorentina.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.