Pata taarifa kuu
CHAN 2018-CAF

Morocco na Sudan zafuzu robo fainali michuano ya CHAN

Timu ya taifa ya Morocco ikisherehekea baada ya kushinda mechi yake ya pili dhidi ya Guinea Januri 17 2018
Timu ya taifa ya Morocco ikisherehekea baada ya kushinda mechi yake ya pili dhidi ya Guinea Januri 17 2018 www.cafonline.com

Wenyeji Morocco imefuzu katika hatua ya robo fainali kuwania taji la CHAN kwa wachezaji wanocheza soka katika ligi za nchi zao. 

Matangazo ya kibiashara

Hatua hii ilikuja baada ya timu hiyo kushinda mechi yake ya pili dhidi ya Guinea kwa kuifunga mabao 3-1.

Ayoub El Kaabi alikuwa kinara wa mchuano kwa kufunga mabao yite matatu katika dakika ya 27, 65 na 68.

Bao pekee ya Guinea ilifungwa na Saidouba Camara katika dakika 29 kipindi cha kwanza na kuondolewa katika michuaono hiyo baada ya kupoteza mechi yake ya pili.

Sudan nayo ilijikatia tiketi kutoka kundi hilo baada ya kuishinda Mauritania bao 1-0 katika mechi yake ya pili.

Morocco inaongoza kundi la A kwa alama 6 sawa na Sudan, huku Guinea na Mauritania ikiwa haina alama yoyote.

Mechi za mwisho za kundi hili zitachezwa siku ya Jumapili mjini Casablanca.

Ratiba Januari 21 2018:-

  • Sudan v Morocco
  • Mauritania v Guinea

Siku ya Alhamisi, michuano ya pili ya kundi B zitachezwa katika uwanja wa Marrakech.

Uganda ambayo ilianza vibaya kwa kufungwa na Zambia mabao 3-1, itamenyana na Namibia huku Ivory Coast nayo ikimenyana na Zambia.

Kund hili linaongozwa Zambia ambayo ina alama tatu, sawa na Namibia.

Michuano ya Alhamisi usiku, ni muhimu kwa Ivory Coast na Uganda ambazo zinahitaji ushindi ili kujipa matumaini ya kusonga mbele.

Ratiba Januari 22 2018:- Kundi C

  • Libya v Nigeria
  • Rwanda v Equitorial Guinea
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.