Pata taarifa kuu
CHAN 2018-CAF

Libya yailemea Rwanda dakika za lala salama kufuzu robo fainali

Mchezaji wa timu taifa ya Libya wakati wa mchuano dhidi ya Rwanda Januari 25 2018
Mchezaji wa timu taifa ya Libya wakati wa mchuano dhidi ya Rwanda Januari 25 2018 www.cafonline.com

Libya imefuzu katika hatua ya robo fainali, kuwania taji la CHAN kwa wachezaji wa bara Afrika wanaocheza soka nyumbani baada ya kupata ushindi muhimu katika dakika za majeruhi dhidi ya Rwanda katika mchuano wa kundi C, uliochezwa Jumanne usiku.

Matangazo ya kibiashara

Elmutasem Abushnaf ndiye aliyewawezesha mabingwa hao wa mwaka 2014 kufika katika hatu hiyo baada kutawala mchezo huo lakini kuonekana kukosa nafasi kadhaa za kufunga goli.

Libya walikwenda katika mchuano huo wakiwa na uhitaji mkubwa wa kushinda na kupata alama tatu muhimu ili kusonga mbele, lakini Rwanda walihitaji tu sare.

Amavubi Stars, walitawala mchezo huo kipindi cha kwanza lakini wakashindwa kupata bao la mapema dhidi ya wapinzani wao ambao walirejea kipindi cha pili na kufanya mashambulizi ya mara kwa mara.

Rwanda, inarejea nyumbani baada ya kushindwa kusonga mbele baada ya kumaliza katika nafasi ya tatu kwa alama 4 nyuma ya Libya ambayo ina alama 6 na Nigeria kuongoza kwa alama 7.

Vijana wa kocha Antoine Hey walianza michuano hii kwa kutofungana na Nigeria lakini ikaifunga Equiorial Guinea kwa bao 1-0.

Libya imeungana na Nigeria hatua ya robo fainali ya michuano hii.

Jumanne usiku, michuano ya kumaliza kundi D zitachezwa katika uwanja wa Adrar na Ibn Batouta.

Mchuano mkali unatarajiwa kuwa kati ya Burkina Faso na Cameroon, kwa sababu Burkina faso wanahitaji ushindi ili kusonga mbele, ina alama moja katika kundi hilo.

Angola ambao watamenyana na Congo Brazil ambayo imefuzu inahitaji tu sare ili kusonga mbele kwa sababu tayari ina alama 4.

Ratiba ya robo fainali, Jumamosi Januari 27 2018:-

Morocco v Namibia

Zambia v Sudan

Januari 28 2018

Mshindi wa kund D v Libya

Nigeria vs Mshindi wa pili kundi D

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.