Pata taarifa kuu
CHAN 2018-ROBO FAINALI

Angola yafuzu robo fainali michuano ya CHAN baada ya kutofungana na Congo

Angola ikipambana na Congo Brazaville Januri 24 2018
Angola ikipambana na Congo Brazaville Januri 24 2018 www.cafonline.com

Timu ya taifa ya Angola, imekuwa ya mwisho kufuzu hatua ya robo fainali kuwania taji la CHAN kwa wachezaji wanaocheza soka katika ligi za nyumbani barani Afrika.

Matangazo ya kibiashara

Angola ilihitaji sare kufika katika hatua hiyo muhimu na kutofungana na Congo Brazaville kumeisaidia na hivyo kumaliza katika nafasi ya pili katika kundi la D kwa alama 5.

Congo Brazaville imemaliza ya kwanza katika kundi hili, na kufuzu baada ya kupata alama 7 kwa kushinda mechi ya kwanza dhidi ya Cameroon bao 1-0 na baadaye dhidi ya Burkina Faso mabao 2-0.

Burkina Faso ambayo imeondolewa katika michuano huu, ilihitaji ushindi na kupata alama tatu muhimu baada ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Cameroon.

Mohammed Sylla alianza vema katika kipindi cha kwanza kwa kuipa bao la ufunguzi Burkina Faso katika dakika ya 43 kipindi cha kwanza, lakini Cameroon ilijikakamua kipindi cha pili na kupata bao la kusawazisha kupitia Patrick Moussombo kusawazisha katika dakika 52 kipindi cha pili.

Ratiba ya michuano ya robo fainai :-

Januari 27 2018

Morocco v Namibia

Zambia v Sudan

Januari 28 2018

Congo v Libya

Nigeria v Angola

 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.