Pata taarifa kuu
RWANDA-SOKA-FERWAFA-CHAN 2018

Antoine Hey aomba kuacha kuifunza Amavubi Stars

Kocha wa timu ya taifa ya Rwanda Antoine Hey
Kocha wa timu ya taifa ya Rwanda Antoine Hey Kigali Today

Shirikisho la soka nchini Rwanda (FERWAFA) limekubali kuvunja mkataba wa kocha wa timu ya taifa Mjerumani Antoine Hey.

Matangazo ya kibiashara

Hey amewaomba viongozi wa soka nchini Rwanda wamruhusu aondoke baada ya matokeo mabaya katika michuano ya CHAN kutafuta ubingwa wa bara Afrika kwa wachezaji wanaocheza katika ligi za nyumbani.

Amavubi Stars waliondolewa katika hatua ya makundi ya michuano hiyo inayoendelea nchini Morocco. Haikufungana na Nigeria, ikaifunga Equatorial Guinea bao 1-0 na kupoteza mchuano wake wa mwisho dhidi ya Libya kwa kulazwa bao 1-0.

Kocha Hey anaondoka Rwanda, licha ya kusalia na miezi miwili katika mkataba aliotia saini na viongozi wa soka nchini Rwanda mwezi Machi mwaka 2017.

Rais wa FERWAFA Vincent Nzamwita amesema pamoja na kwamba wamekubali ombi la Hey, itabidi atekeleze matakwa ya mkataba huo kwa uamuzi wake wa kuondoka mapema.

Ripoti zinasema kuwa, huenda Hey akaenda kuifunza timu ya taifa ya Syria baada ya kuondoka Rwanda.

Amewahi pia kuifunza Kenya, Lesotho na Gambia.

Acheni niondoke, Antoine Hey aiambia FERWAFA.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.