Pata taarifa kuu
MANCHESTER CITY-LIVERPOOL-MICHEZO-SOKA

Ligi ya Mabingwa: AS Roma yaiburuza Barcelona, Liverpool yaizamisha City

Mlinzi kutoka Ugiriki Kostas Manolas baada ya kufunga bao la tatu la AS Roma sawa na kutinga nusu fainali Aprili 10, 2018.
Mlinzi kutoka Ugiriki Kostas Manolas baada ya kufunga bao la tatu la AS Roma sawa na kutinga nusu fainali Aprili 10, 2018. REUTERS/Tony Gentile

Baada ya kufungwa mabao 4-1 katika mechi yao ya awali ya robo fainali dhidi ya Barcelona, AS Roma imefaulu kupiga hatua mbele kwa kufunga mabao 3-0 wakati wa mechi ya marudiano kwenye uwanja wa Stadio Olimpico. Itakua mara ya kwanza kwa klabu hii kuingia nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa tangu mwaka 1984.

Matangazo ya kibiashara

Katika mchezo mwengine uliopigwa siku ya Jumanne, Aprili 10, Liverpool pia amefanikiwa tena kupata ushindi dhidi ya Manchester City kwa mabao 2-1, bao lilifungwa na nyota kutoka Misri Mohamed Salah.

Liverpool imefika katika nusu fainali yao ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa kwa miaka 10. Kwa mechi mbili zote kwa ushindi wa jumla, Liverpool imeibwagiza Man City mabao 5-1.

Magoli ya Liverpool yaliingizwa na Mohamed Salah baada ya mbio za nguvu kutoka kwa Sadio Mane mnamo dakika ya 56.

Goli hilo lilimfanya Salaha kuwa na magoli39 katika msimu huu.

Goli la pili lilifungwa na Robert Firmino dakika 13 kabla ya kumalizika kwa mchezo.

Leo kuna michuano ya pili ya robo fainali. Bayern Munich ya Ujerumani watakuwa nyumbani kuwakabili Sevilla ya Uhispania.

Mechi ya kwanza, Bayern Munich walishinda kwa mabao 2-1. Nao mabingwa mara 12 wa michuano hii Real Madrid, watakuwa nyumbani kumenyana na Juventus ya Italia. Mechi ya kwanza, Real Madrid walipata ushindi wa mabao 3-0.

Mechi zote zitachezwa kuanzia saa tatu na dakika 45 saa za Afrika Mashariki.

Washindi wataungana na AS Roma na Liverpool katika hatua ya nusu fainali.

 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.