Pata taarifa kuu
CAF-AFRIKA-SOKA

CAF yafanya mabadiko kwenye ratiba ya michuano

Nembo za mashindano ya CAF
Nembo za mashindano ya CAF RFI Kiswahili

Shirikisho la soka barani Afrika CAF limefanya mabadiliko ya siku za kuchezwa michuano ya klabu bingwa na Shirikisho barani Afrika.

Matangazo ya kibiashara

Michuano ya klabu bingwa sasa itakuwa inachezwa siku za Ijumaa, Jumamosi na siku za Jumanne katikati ya wiki.

Siku za Jumapili na Jumatano, itakuwa ni zamu ya michuano ya taji la Shirikisho.

Amr Fahmy, Katibu Mkuu wa CAF amesema mabadiliko hayo yanalenga kuwashawishi mashabiki kufika uwanjani lakini pia kuimarisha mashindano hayo ili kufahamika zaidi duniani.

Mabadiliko haya yataanza kutekelezwa wakati wa michuano ya hatua ya makundi msimu huu.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.