Pata taarifa kuu
BAYERN MUNICH-REAL MADRID-SOKA

Bayern Munich kumenyana na Real Madrid

Kikosi cha wachezaji wa Bayern Munich, Ogasti 5, 2015
Kikosi cha wachezaji wa Bayern Munich, Ogasti 5, 2015 REUTERS/Michaela Rehle

ayern Munich watamenyana na mabingwa mara 12 wa michuano hii Real Madridi. Mechi hii itachezwa saa tatu na dakika 45 usiku saa za Afrika Mashariki katika uwanja wa Allianz Arena.

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo, Bayern Munich huenda ikamkosa beki wake David Alaba lakini kocha anatarajiwa kufanya maamuzi kuhusu hatima ya mchezaji huyo.

Mchezahi wa Bayern MunichDavid Alaba.
Mchezahi wa Bayern MunichDavid Alaba. REUTERS/Michael Dalder

Kwa upande wa Real Madrid, kiungo wa Kati James Rodriguez anatarajiwa kuanza mechi ya leo baada ya kuonekana kuwa kiungo muhimu katika klabu hiyo.

Hii itakuwa mara ya tatu kwa Bayern Munich na Real Madrid kukutana katika hatua ya nusu tangu mwaka 2011.

Jumanne usiku wiki hii, Liverpool ilianza vema nyumbani baada ya kupata ushindi mkubwa wa mabao 5-2 katika uwanja wake wa Anfield na sasa inasubiri mchuano wa marudiano tarehe 2 mwezi ujao.

Mohammed Salah na Roberto Firmino waliifungia timu yao mabao mawili kila mmoja akifunga bao lake huku Sadio Mane naye akiingia katika vitabu vya ufungaji wa mabao katika klabu hiyo.

Edin Dzeko na Diego Perotti, waliifungia AS Roma.

 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.