Pata taarifa kuu
BAYERN MUNICH-REAL MADRID-SOKA

Real Madrid yailaza Bayern Munich

Mchezaji kutoka Brazil Marcelo, akizungukwa na wachezaji wenzake wa Real Madrid, baada ya kuilaza Bayern Munich tarehe 25 Aprili, 2018.
Mchezaji kutoka Brazil Marcelo, akizungukwa na wachezaji wenzake wa Real Madrid, baada ya kuilaza Bayern Munich tarehe 25 Aprili, 2018. Kai Pfaffenbach/Reuters

Real madrid imeikomoa Bayern Munich katika mtanange wa mkondo wa kwanza wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa kwa mabao 3-1. Ronaldo hakupata fursa ya kushambulia katika mechi hiyo , ikiwa ni mara ya kwanza kwa yeye kushindwa kufanya hivyo katika kombe la vilabu bingwa tangu Mei 2017.

Matangazo ya kibiashara

Mchuano huu kati ya Bayern Munich na Real Madrid ulikuwa mchuano wa kupigania pia ubabe wa soka la Ulaya. Kidumbwedumbwe hicho cha kwanza kati ya timu hizo mbili kilipigwa katika uga wa Allianz Arena.

Bayern sasa watalazimika kufunga mabao mawili Jumanne ijayo ili kuwazuia Real Madrid kufika fainali ya nne katika kipindi cha miaka mitano

Mabao ya Real Madrid yalifungwa na Marcelo na Asensio katika kila kipindi cha mchezo. Na Rifinha kufanya masikhara kuwapatia bao la ugenini.

Hii ilikuwa mara ya 25 kwa timu hizo mbili kukutana katika soka ya Ulaya, huku kila timu ikiwa imeshinda mara 11 na kutoka sare mara mbili. Jana usiku ilikuwa mara ya saba kwa vilabu hivi kukutana katika nusu fainali. Katika mapambano yao yote, Real Madrid imefunga jumla ya mabao 37, Bayern mabao 36. 

Awali kocha wa Bayern Munich Jupp Heynckes amesema Real Madrid inapaswa kuwa na wasiwasi kuhusu Robert Lewandowski kama vile ambavyo Bayern Munich itakuwa inalenga kumdhibiti Cristiano Ronaldo.

Mabingwa hao wa Ujerumani waliwaalika Real katika mechi kali ya miamba ya Ulaya wakilenga kutwaa mataji matatu msimu huu. 

Ronaldo amefunga mabao 42 katika mechi 39 wakati Lewandoswki ametikisa wavu mara 39 katika mechi 43. Mechi ya marudio ya nusu fainali kati ya timu hizo mbili itakuwa Mei mosi mjini Madrid.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.