Pata taarifa kuu
LIVERPOOL-AS ROMA-SOKA

Liverpool kuburuzana na AS Roma Jumatato hii

Mshambuliaji wa Liverpool Sadio Mané akiwa na wachezaji wenzake.
Mshambuliaji wa Liverpool Sadio Mané akiwa na wachezaji wenzake. Carl Recine / Reuters

Klabu ya Liverpool Jumatano usiku inamenyana na AS Roma katika mchuano wa marudiano kufuzu hatua ya fainali kutafuta taji la klabu bingwa barani Ulaya.

Matangazo ya kibiashara

Liverpool ilianza vema nyumbani baada ya kupata ushindi mkubwa wa mabao 5-2.

Hata hivyo, kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amewaonya wachezaji wake kuwa makini ugenini watakapocheza mechi hiyo katika uwanja wa Olimpico nchini Italia.

Liverpool ambao wapo katika nafasi nzuri ya kufuzu katika fainali yake ya nane na ya kwanza tangu mwaka 2007, inahitaji kuwa makini ili kuepuka adhabu iliyopata Barcelona katika hatua ya robo fainali ya michuano hii.

Barcelona waliokuwa wamepata ushindi katika mechi ya mzunguko wa kwanza, lakini wakazidiwa katika mechi ya pili ugenini.

AS Roma wanatarajiwa kuleta furaha kwa mashabiki wake baada ya Italia kushindwa kufuzu kombe la dunia nchini Urusi.

Mshindi wa mechi ya leo atakutana na Real Madrid ambayo ilifuzu fainali hapo jana baada ya kuishinda Bayern Munich kwa jumla ya mabao 4-3.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.