Pata taarifa kuu
AMERIKA-SOKA-MICHEZO

Nchi za Amerika Kaskazini zatakiwa kuonyesha umoja kuelekea Kombe la dunia 2026

Carlos Tevez, mchezaji wa Argentina wakati wa Kombe la Dunia la mwaka 2010.
Carlos Tevez, mchezaji wa Argentina wakati wa Kombe la Dunia la mwaka 2010. JEWEL SAMAD / AFP

Viongozi wa mataifa ya Amerika Kaskazini wametoa wito kwa wapiga kura, kutotilia maanani masuala ya siasa katika nchi hizo kuelekea upigaji kura wa Marekani, Canada na Mexico kuwa wenyeji wa kombe la dunia katika mchezo wa kandandaa mwaka 2026.

Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huo utafanywa mwezi ujao jijini Moscow nchini Urusi, kabla ya kuanza kwa michuano ya kombe la dunia.

Rais wa Shirikisho la soka nchini Marekani Carlos Cordeiro, akizungumza na wanahabari wa michezo jijini Brussels, amesema iwapo mataifa hayo yatapata nafasi hiyo, Shirikisho la soka duniani FIFA litapata faida ya Dola Bilioni 11, toka Dola Bilioni 2.6 kama ilivyokuwa nchini Brazil mwaka 2016.

Marekani, Canada na Mexico, zinapambana na Morocco kuwania nafasi hiyo ya kihistoria.

Morocco nayo imeendelea kuomba kura, huku mataifa ya Afrika na yale ya bara Asia yakisema yataunga mkono taifa hili la Kaskazini mwa Afrika. Jibu litakuwa wazi tarehe 13 mwezi ujao.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.