Pata taarifa kuu
FIFA-URUSI-KOMBE LA DUNIA 2018

Fahamu Kundi E, fainali ya kombe la dunia 2018

Kundi E
Kundi E FIFA.COM

Kundi EKundi hili lina timu za Brazil, Uswizi, Costa Rica na Serbia.Muhimu:- Mchuano wa ufunguzi katika kundi hili, utakuwa kati ya Brazil na Uswizi tarehe 17 mwezi Juni katika uwanja wa Rostov Arena.Wachambuzi wa soka wanasema hili ni miongoni mwa kundi gumu katika michuano hii.

Matangazo ya kibiashara

Brazil

Timu ya taifa ya Brazil
Timu ya taifa ya Brazil FIFA.COM

Brazil imefuzu mara 20 katika michuano ya historia ya kombe la dunia.

Mara ya kwanza, ilikuwa ni mwaka 1930 na mara ya mwisho ilikuwa ni mwaka 2014, walipokuwa wenyeji.

Wameshinda taji la kombe la dunia mara tano mwaka 1958, 1962, 1970, 1994 na 2002.

Imefika katika hatua ya nusu fainali mara 11 na fainali mara saba.

Mchezaji wa kuangaliwa katika kikosi cha Brazil mshambuliaji Neymar. Yatakuwa ni mashindano yake ya pili baada ya kuichezea timu yake mwaka 2014.

Kocha wa sasa ni Adenor Leonardo Bacchi maarufu kama Tite. Ni raia wa Brazil ambaye amekuwa akiifunza Brazil mwaka 2016.

Uswisi

Timu ya taifa ya Uswizi
Timu ya taifa ya Uswizi FIFA.COM

Imeshiriki katika michuano 10 ya kombe la dunia katika historia yake ya mchezo wa soka.

Ilishiriki mara ya kwanza mwaka 1934 na mara ya mwisho ilikuwa ni mwaka 2014.

Matokeo mazuri yalionekana katika hatua ya robo fainali mwaka 1934, 1938 na 1954.

Haijawahi kufika katika hatua ya nusu fainali au hata fainali.

Kocha wa timu hii ni Vladimir Petkovic, raia wa Uswisi mwenye asili ya Bosnia.

Mchezaji wa kuangaliwa katika kikosi cha Uswisi ni mshambuliaji Granit Xhaka, anayecheza katika klabu ya Arsenal nchini Uingereza.

Costa Rica

Timu ya taifa ya Costa Rica
Timu ya taifa ya Costa Rica FIFA.COM

Imecheza katika michuano nne ya kombe la dunia, mara ya kwanza ikiwa ni mwaka 1990 na mwisho ikiwa ni mwaka 2014.

Mwaka 2014, ilikuwa mara ya kwanza kwa nchi hiyo kufika katika hatua ya robo fainali.

Kocha wa timu hii ni Oscar Ramirez tangu mwaka 2015. Aliwahi pia kuwa naibu kocha wa timu hii.

Alikuwa kiungo wa kati wa zamani wa timu hii na hata kuiwakilisha nchi yake katika fainali ya kombe la dunia nchini Italia mwaka 1990.

Mchezaji hatari na wa kuangaliwa katika fainali hii ni Bryan Ruiz, ambaye aliisaidia sana timu yake kufuzu katika kombe la dunia kwa kufunga mabao matatu.

Serbia

Timu ya taifa ya Serbia
Timu ya taifa ya Serbia FIFA.COM

Imewahi kufuzu katika michuano ya kombe la dunia mara 11. Mara ya kwanza ilikuwa ni mwaka 1930 na mara ya mwisho ilikuwa ni mwaka 2010 nchini Afrika Kusini.

Nafasi nzuri ambayo imewahi kufika ilikuwa ni katika nafasi ya nne, wakati wa fainali za mwaka 1930 na 1962.

Hatua ya nusu fainali imefika mara mbili katika historia yake ya mashindano haya.

Kocha wa sasa wa timu hii ni mchezaji wa zamani Mladen Krstajic. Mwaka 2006 aliichezea timu yake ya taifa wakati wa michuano ya kombe la dunia nchini Ujerumani.

Mchezaji wa kuangaliwa sana katika timu hii ni nahodha Branislav Ivanovic.

Ivanovic, amekuwa nahodha tangu mwaka 2012 na akicheza soka la kulipwa nchini Uingereza, amewahi kuisadia Chelsea kunyakua taji la ligi kuu la lile la klabu bingwa barani Ulaya.

 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.