Pata taarifa kuu

Zinedine Zidane: Naamua kutoendelea kuinoa Real Madrid mwaka ujao

Zinedine Zidane,kocha wa Reala Madrid, achukua uamuzi wa kutoendelea kuinoa klabu hiyo.
Zinedine Zidane,kocha wa Reala Madrid, achukua uamuzi wa kutoendelea kuinoa klabu hiyo. Juan Medina/Reuters

Katika mkutano na waandishi wa habari, kocha wa Real Madrid, raia wa Ufaransa, Zinedine Zidane ametangaza kuwa hatoendelea kuinoa klabu hiyo mwaka ujao. Uamzi huo unakuja siku chache tu baada ya klabu hii kutwaa Kombe la Ligi ya Mabingwa.

Matangazo ya kibiashara

"Nimechukua uamuzi wa kutoendelea mwaka ujao kama kocha wa Real Madrid, " Zinedine Zidane amesema Alhamisi hii Mei 31.

Zinedine Zidane alianza kuinoa klabu ya Real Madrid tangu mwanzoni mwa mwaka 2016.

Uamuzi wa Bw Zidane unashangaza wengi, kwani hatukua tunautarajia", amesema rais wa klabu hiyo Uhispania, Florentino Perez.

Zinedine Zidane amesema ameamua kustafu na "hakuna klabu yoyote ambayo anatarajia kuinoa".

Zinedine Zidane, kocha ambaye alianza kuinoa klabu hii tangu mwanzoni mwa mwaka 2016, amekua kocha wa kwanza kushinda Ligi ya Mabingwa mara tatu mfululizo, ikiwa ni uzoefu wake wa kwanza kwa timu hii ya kimataifa ya wachezaji nyota.

Alikua amesaini mkataba mnamo mwezi Januari 2016 kuinoa Real Madrid hadi mwaka 2020.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.