Pata taarifa kuu
FIFA-URUSI-SOKA

Wajumbe wa FIFA kuamua nani atakuwa mwenyeji wa fainali za mwaka 2026

Wajumbe kutoka nchi wanachama 207 wanaokutana jijini Moscow, Urusi wana uamuzi mmoja tu, nao ni kutumia kura yao kuamua nani atakuwa mwenyeji wa fainali za mwaka 2026.
Wajumbe kutoka nchi wanachama 207 wanaokutana jijini Moscow, Urusi wana uamuzi mmoja tu, nao ni kutumia kura yao kuamua nani atakuwa mwenyeji wa fainali za mwaka 2026. Flickr-Gamescom EA Sports FIFA18

Wajumbe wa shirikisho la Soka Duniani, FIFA, baadae Jumatano wiki hii, watapiga kura kuchagua nchi ambayo itakuwa mwenyeji wa fainali za kombe la dunia za mwaka 2026, ushindani ukiwa ni kati ya nchi ya Morocco inayoungwa mkono na nchi za Afrika na nchi 3 za Amerika zinazoungwa mkono na nchi za Ulaya.

Matangazo ya kibiashara

Wajumbe kutoka nchi wanachama 207 wanaokutana jijini Moscow, Urusi wana uamuzi mmoja tu, nao ni kutumia kura yao kuamua nani atakuwa mwenyeji wa fainali za mwaka 2026.

Nchi za Marekani, Canada na Mexico kwa pamoja zimeomba kuwa waandaaji wa fainali hizi na zinaonekana kuongoza katika uwezekano wa kushinda zabuni hii kutokana na miundo mbinu mizuri na usafiri wa uhakika.

Hata hivyo zabuni ya Morocco inaonekana kuwa kwenye makaratasi zaidi huku viwanja vingi vikiwa havijajengwa na wengi wanahoji ni namna gani nchi hiyo itaweza kwenda na kasi ya fainali za mwaka huo ambapo timu zitakuwa 48 kutoka 32 za sasa.

Wakaguzi wa FiFA wamesema viwanja, hoteli na miundo mbinu ya usafiri ni hatarishi, ambapo waliipa alama 2.7 kati ya alama 5 huku wakionesha wasiwasi katika maeneo kadhaa.

Marekani ilipoteza kwa Qatar itakayoandaa fainali za mwaka 2022, hatua iliyosababisha kubadilishwa kwa sheria za upigaji kura, ambapo awali wajumbe 24 wa kamati ya utendaji walikuwa wanaamua nani ataandaa, lakini safari hii wajumbe wote wa Fifa watapiga kupata mshindi.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.