Pata taarifa kuu
KOMBE LA DUNIA-ENGLAND-URUSI

England yavunja rekodi ya miaka 28

Kipa wa  England Jordan Pickford akiokoa mchomo langoni kwake wakati wa mechi ya robo fainali dhidi ya Sweden
Kipa wa England Jordan Pickford akiokoa mchomo langoni kwake wakati wa mechi ya robo fainali dhidi ya Sweden REUTERS/David Gray

Baada ya miaka 28 timu ya taifa ya England imefuzu kucheza hatua ya nusu fainali ya kombe la dunia baada ya hapo jana kuilaza Sweden mabao 2-0.

Matangazo ya kibiashara

Mabao ya England yalifungwa na Harry Maguire na Dele Ali kila kipindi na kukihakikishia kikosi cha Gareth Southgate kufika hatua hiyo.

Mara ya mwisho kwa England kufuzu hatua ya nusu fainali ya Kombe la dunia ilikuwa mwaka 1990, michuano iliyofanyika nchini Italia.

England imeshinda mara moja Kombe la dunia, mwaka 1966 walipoandaa na watachuana na Croatia ambayo jana pia iliwaondoa wenyeji Urusi kwa mikwaju ya penati 4-3.

 

 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.