Pata taarifa kuu
REAL MADRID-CHRISTIANO RONALDO-LUKA MODRIC

Modric: Ninaamini Ronaldo atasalia Santiago Bernabeu

Nahodha wa Timu ya Taifa ya Croatia,Luka Modric
Nahodha wa Timu ya Taifa ya Croatia,Luka Modric REUTERS/Darren Staples

Nahodha wa Timu ya Taifa ya Croatia Luka Modric amesema anaamini mchezaji mwenzake katika klabu ya Real Madrid atasalia kuitumikia Real Madrid.

Matangazo ya kibiashara

Kumekuwa na ripoti kadhaa zinazochapishwa na vyombo vya habari barani Ulaya zikimhusisha Ronaldo kuihama Madrid inayotumia Uwanja wa Santiago Bernabeu na kujiunga na miamba ya soka nchini Italia, Juventus.

Akizungumza na mtandao wa sky Sports baada ya kuiongoza Croatia kufuzu nusu fainali ya Kombe la dunia mchezaji huyo amesema ana imani kuwa Ronaldo atamalizia soka lake akiwa Rela Madrid.

“Sifikiri kama ataondoka, na ningependa kumwona akibaki kwa sababu yeye ni mchezaji bora duniani. Sifikiri kumuona katika timu nyingine ya Ulaya,”amesema Modrc ambaye sambamba na Ronaldo wameshinda mataji manne ya Ligi ya mabingwa Ulaya wakiwa Rela madrid.

 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.