Pata taarifa kuu
CAF-SHIRIKISHO-GOR MAHIA-YANGA

Gor Mahia FC yaivunja moyo Yanga mchuano muhimu wa taji la Shirikisho Afrika

Wachezaji wa Gor Mahia wakisherehekea baada ya kuishinda Yanga ya Tanzania mabao 4-0 Julai 18 2018
Wachezaji wa Gor Mahia wakisherehekea baada ya kuishinda Yanga ya Tanzania mabao 4-0 Julai 18 2018 www.cafonline.com

Gor Mahia ya Kenya siku ya Jumatano usiku iliandikisha ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Young Africans ya Tanzania katika mchuano muhimu wa hatua ya makundi kuwania taji la Shirikisho barani Afrika.

Matangazo ya kibiashara

Ephrem Guikan mchezaji wa kulipwa kutoka Ivory Coast alifunga mabao mawili katika mchuano huo huku mabao mengine yakitiwa kimyani na Jacques Tuyisenge huku Haji Mwinyi akijifunga.

Matokeo haya yanatoa nafasi kubwa mabingwa hao wa taji hili mwaka 1987, kufuzu katika hatua ya robo fainali.

Gor Mahia sasa ni ya pili katika kundi D, kwa alama 5 nyuma ya  USM Alger ya Algeria ambayo ina alama 7 baada ya kuifunga Rayon Sport ya Rwanda mabao 2-1.

Mechi nyingine ya kundi hili, itachezwa tarehe 29 Julai. Gor Mahia watakuwa wageni wa Yanga jijini Dar es salaam huku USM Alger wakichuana na Rayon Sport.

Matokeo mengine katika michuano hii:-

Enyimba 1-0 Williamsville AC

Djoliba 2-0 CARA Brazzaville

Al-Hilal 2-2 UD Songo

RS Berkane 0-0 Al-Masry

Aduana Stars 2-1 AS Vita Club

ASEC Mimosas 0-1 Raja Casablanca

 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.