Pata taarifa kuu

Ethiopia na Eritrea kucheza mechi ya kirafiki mnamo mwezi Agosti

Bendera za Ethiopia na Eritrea katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole huko Addis Ababa, Ethiopia mnamo 26 Juni, 2018..
Bendera za Ethiopia na Eritrea katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole huko Addis Ababa, Ethiopia mnamo 26 Juni, 2018.. REUTERS/Tiksa Negeri

Ethiopia na Eritrea wanatarajia kucheza mechi ya soka ya kirafiki katika mji mkuu wa Eritrea, Asmara, mwishoni mwa mwezi Agosti, shirika la habari la serikali ya Ethiopia Fana limearifu.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hiyo inakuja baada ya viongozi wa nchi hizi mbili kutia saini kwenye makubaliano yanayositisha miaka ishirini ya vita kati ya nchi hizo mbili mapem amwezi huu wa Julai.

Mechi hii ni sehemu ya jijuhudi za Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed zinazolenga kuboresha maridhiano baada ya nchi hizi mbili jirani kukumbwa na uhasama uliodumu miongo miwili.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed na Rais Eritrea Isaias Afwerki walitia saini taarifa ya pamoja ya amani na urafiki" tarehe 9 Julai katika mji wa Asmara. Jambo ambalo liliashiria kusitishwa kwa miaka ishirini vita kati ya nchi hizi mbili jirani.

Kusainiwa kwa makubaliano hayo kulitokana na mkutano wa kihistoria kati ya viongozi hawa wawili katika mji mkuu wa Eritrea.

Kati ya mwaka 1998 na 2000, kutokana na mgogoro wa kweningia katika vita ambavyo vimeua watu 80,000.

Eritrea ilipata uhuru mwaka 1993 baada ya miaka 30 ya vita dhidi ya utwala wa Ethiopia. Mpaka wa pamoja unaendelea kulindwa na majeshi kutoka pande mbili.

Mwaka 2002, Mahakama ya kudumu ya Usuluhishi ya Hague ilitoa uamuzi kwamba mji wa Badme ni sehemu ya Eritrea lakini Addis Ababa ilipuuzia mbali uamuzi huo na mji wa Badme unaendelea kuwa chini ya utawala wa Ethiopia.

Abiy Ahmed, ambaye alichukua madaraka yuko tayari kuheshimu uamuzi huo wa mahakam ya kimataifa.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.