Pata taarifa kuu
KENYA-ARGENTINA-OLIMPIKI 2018-MAGONGO

Kenya yaanza vibaya mashindano ya Olimpiki 2018 kwa vijana

Timu ya taifa ya mchezo wa magongo ya Kenya
Timu ya taifa ya mchezo wa magongo ya Kenya olympic games 2018

Kenya imeanza vibaya mashindano ya vijana ya Olimpiki yanayoendelea nchini jijini Buenos Aires nchini Argentina, baada ya kufungwa na Australia mabao 7-0 katika mchezo wa magongo.

Matangazo ya kibiashara

Mabao ya Australia yalifungwa na James Collins na Miles Davis, waliofunga mabao mawili kila mmoja huku Lain Carr, Allistair Murray na Ben White wakiifunga Kenya.

Kocha Kevin Lugalia amesema vijana wake wamepata matokeo haya mabaya kutokana na woga na  wasiwasi wakati wa mchuano huo.

Hii ndio ya kwanza Kenya inashiriki katika mchezo wa magongo kushiriki katika mashindano haya ya Olimpiki kwa vijana kwa wachezaji watano kila upande.

Mbali na mchuano huo, Kenya itachuana na Canada, India, Bangladesh na Austria.

Wawakilishi wengine wa Afrika Zambia, nayo ilianza vibaya baada ya kufungwa na Argentina mabao 6-2.

Imepangwa pia na Malaysia, Mexico, Poland na Vanuatu.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.