Pata taarifa kuu
SOKA-VIJANA-TANZANIA-AFCON 2019

Droo ya michuano ya soka kwa vijana barani Afrika kutolewa

Michuano ya vijana wasiozidi miaka 17
Michuano ya vijana wasiozidi miaka 17 CAF Online

Droo ya michuano ya bara Afrika, kuwania taji la vijana wasiozidi miaka 17 itafanyika siku ya Alhamisi jijini Dar es salaam nchini Tanzania.

Matangazo ya kibiashara

Michuano hiyo ya 13, itafanyika jijini Dar es salaam nchini Tanzania kati ya tarehe 14 hadi 28 mwezi Aprili mwaka 2019.

Wenyeji Tanzania, ni miongoni mwa mataifa nane, yaliyofuzu kucheza katika fainali hiyo.

Mataifa mengine yatakayopambana kutafuta ubingwa huo ni pamoja na Morocco, Senegal, Guinea, Nigeria, Cameroon, Uganda na Angola.

Mataifa yatakayofika katika hatua ya nusu fainali, yatafuzu kushiriki katika kombe la dunia mwaka 2019 nchini Peru.

Mabingwa watetezi Mali, walishindwa kufuzu katika fainali ya mwaka 2019.

Uganda nayo inashiriki katika michuano hii kwa mara ya kwanza.

 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.