Pata taarifa kuu
SOKA-AFRIKA

Gor Mahia waongoza nafasi ya pili shingo upande

Klabu ya Kenya ya Gor Mahia.
Klabu ya Kenya ya Gor Mahia. Twitter. com/ Gor Mahia

Klabu ya Kenya Gor Mahia imeadhibiwa na klabu ya Algeria, NA Hussein Dey, katika michi iliyopigwa Jumapili katika uwanja wa jijini Algiers, nchini Algeria.

Matangazo ya kibiashara

Bao la kusawazisha la Klabu ya Gor Mahia kutoka nchini Kenya, limekataliwa katika mechi ya hatua ya makundi kuwania taji la Shirikisho barani Afrika dhidi ya timu ya NA Hussein Dey Jumapili usiku.

Bao hilo lilikuwa limefungwa na beki kutoka nchini Uganda Shafik Batambuze katika dakika 59 baada ya kuunganishwa kona, na kufanya matokeo kuwa bao 1-1 lakini mwamuzi kutoka nchini Mali Boubou Traore.

Hatua hiyo, iliwakasirisha wachezaji na mashabiki wa Gor Mahia waliokuwa nchini Algiers kushudhudia mechi hiyo.

Mechi hiyo ilikamilika kwa mabingwa wa soka nchini Kenya kupoteza kwa bao 1-0 na kuifanya Na Hussein Dey kuongoza kundi la D kwa alama saba.

Gor Mahia ni ya pili katika kundi hilo kwa alama 6, ikifuatwa na Zamalek ambayo ina alama tano baada ya kuishinda Petro de Luanda ya Angola bao 1-0 .

Al Hilal ya Sudan nayo imeendelea kupata matokeo mazuri baada ya kuishinda ZESCO UNITED ya Zambia kwa mabao 3-1 na inaongoza kundi la C kwa alama 7, ikifuatwa na Asante Kotoko ya Ghana ambayo nayo ilipata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Nkana ya Zambia.

Etoile du Sahel ya Tunisia, nayo ikiwa ugenini iliishinda Enugu Rangers ya Nigeria mabao 2-0 huku Salitas ya Burkina Faso ikatishana nguvu kwa kutofungana na CS Sfaxien.

Kundi A, RS Berkane ya Morocco inaendelea kuongoza kundi hilo kwa alama nane licha ya kutoka 0-0 dhidi ya ndugu zao Raja Casablanca lakini AS Otoho, ya Congo Brazzaville iliishinda Hassania Agadir ya Morocco bao 1-0.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.