Pata taarifa kuu
CAF-SOKA

Mechi kuwania taji la klabu bingwa barani Afrika kupigwa katika viwanja mbalimbali

Mechi zinatarajiwa kushuhudiwa katika nchi mbalimbali barani Afrika Ijumaa Machi 8 na 9, 2019.
Mechi zinatarajiwa kushuhudiwa katika nchi mbalimbali barani Afrika Ijumaa Machi 8 na 9, 2019. CC BY-SA 2.0 Rafa Otero via Flickr

Michuano ya hatua ya makundi, kuwania taji la klabu bingwa barani Afrika inaendelea leo Ijuma na kesho Jumamosi katika mataifa mbalimbali barani Afrika.

Matangazo ya kibiashara

Orlando Pirates ya Afrika Kusini itacheza na FC Platinum ya Zimbabwe katika mechi ya kundi B, huku Esperance de Tunis ya Tunisia ikimenyana na Horoya ya Guinea.

Kundi C, Ismail ya Misri itamenyana na TP Mazembe ya DRC, huku CS Constantune ya Algeria ikiwa nyumbani kucheza na Club Africain ya Tunisia.

Kesho mechi za kundi D:

AS Vita Club itacheza na Al-Ahly, huku JS Soura ikichuana na Simba FC ya Tanzania.

Kundi A :

ASEC Mimosa ya Cote Dvoire itakuwa nyumbani kucheza na Wydad Casablanca huku Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini ikichuana na Lobi Stars.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.