Pata taarifa kuu
KENYA-FKF-SOKA

FKF na Harambee Stars wapata ufadhili kutoka kampuni ya Betin

Wachezaji wa Harambee Stars wakishangilia baada ya ushindi wa taji CECAFA
Wachezaji wa Harambee Stars wakishangilia baada ya ushindi wa taji CECAFA Goal.com

Shirikisho la soka nchini Kenya FKF limepata ufadhili wa Dola 200, 000 kutoka kwa kampuni ya kubashiri michezo ya Betin sawa na Shilingi za nchi hiyo Milioni 20 kuisaidia timu ya taifa Harambee Stars, kuelekea katika michuano ya bara Afrika nchini Misri mwezi Juni.

Matangazo ya kibiashara

Dola 50,000 zitatumiwa kugharamia jezi ya timu ya taifa wakati wa michuano hiyo ambayo Kenya imerejea baada ya miaka 15.

Habari hii njema imekuja wakati kikosi hicho kikijiandaa kucheza na Ghana katika mechi yake ya mwisho hatua ya makundi tarehe 23 mwezi huu jijini Accra.

Hata hivyo, Kenya itamkosa mshambuliaji wake Michael Olunga ambaye alipata jeraha wakati akiichezea klabu yake ya Kashiwa Reysol, nchini Japan na madaktari wake wanasema hatakuwa amepona kabla ya mechi hiyo muhimu.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.