Pata taarifa kuu
KOMBE LA DUNIA KWA VIJANA-POLAND-TIKETI-AFRIKA

Tiketi zaidi ya 100,000 zauzwa kuelekea kombe la dunia kwa vijana

Kombe la dunia kwa vijana wasiozidi miaka 20 nchini Poland
Kombe la dunia kwa vijana wasiozidi miaka 20 nchini Poland www.fifa.com

Shirikisho la soka duniani FIFA, limesema kuelekea fainali ya kombe la dunia kwa vijana wasiozidi miaka 20, tayari tiketi zaidi ya 100, 000 zimeuzwa.

Matangazo ya kibiashara

Fainali hiyo itafanyika nchini Poland kati ya tarehe 23 mwez Mei hadi Juni 15 mwaka 2019.

Ripoti zinaonesha kuwa mashabiki wengi wamenunua tiketi za  kushuhudia mechi ya ufunguzi kati ya wenyeji Poland na Colombia itakayochezwa katika uwanja wa Widzewa mjini Lodz.

Wenyeji Poland wamepangwa katika kundi la A pamoja na Colombia, Tahiti na Senegal.

Kundi B: Mexico, Italia, Japan na Ecuador.

Kundi C: Honduras, New Zealand, Uruguay, Norway

Kundi D: Qatar, Nigeria, Ukraine na Marekani

Kundi E: Pana, Mali, Ufaransa, Saudi Arabia

Kundi F: Ureno, Korea Kusini, Argentina, Afrika Kusini

Mataifa 24 yatashiriki katika fainali hizo za 22 na bara la Afrika litawakilishwa na Senegal, Nigeria, Afrika Kusini na Mali.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.