Pata taarifa kuu
MICHEZO-SOKA

Timu nne kujitupa uwanjani katika mechi za kimataifa za kirafiki

Mechi nne za kimataifa za kirafiki zitapigwa Jumatano hii Machi 20 katika viwanja mbalimbali.
Mechi nne za kimataifa za kirafiki zitapigwa Jumatano hii Machi 20 katika viwanja mbalimbali. (Source: UEFA)

Leo Jumatano usiku kutakuwa na mechi tatu za Kimataifa za kirafiki katika mchezo wa soka. Wales, Trinidad and Tobago, Ujerumani na Serbia watajitupa uwanjani.

Matangazo ya kibiashara

Saa nne na dakika 45 saa za Afrika Mashariki (sawa na saa tatu na dakika 45 saa za Afrika ya Kati), Wales watakuwa wenyeji wa Trinidad and Tobago, lakini Ujerumani watakuwa wanamenyana na Serbia.

Mapema kuanzia saa 12 jioni, Iraq watachuana na Syria.

Wakati uo huo, maandalizi ya michuano ya kufuzu kucheza katika fainali ya bara Ulaya maarufu kama UEFA Euro mwaka 2020, inaendelea leo kuelekea mechi kuanza kuchezwa kesho.

Miongoni mwa mechi zitazochezwa kesho ni pamoja na Ubelgiji dhidi ya Urusi, Israel na Slovenia, Austria na Poland, miongoni mwa mengine.

Mabingwa watetezi wa taji hili ni Ureno.

Michuano hiyo itachezwa katika mataifa 12 barani Ulaya kati ya mwezi Juni na Julai.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.