Pata taarifa kuu
TANZANIA-UGANDA-SOKA

Tanzania yaburuzwa na Uganda 3-0

Timu ya taifa ya vijana wasiozidi miaka 17 kutoka Tanzania, Serengeti Boys.
Timu ya taifa ya vijana wasiozidi miaka 17 kutoka Tanzania, Serengeti Boys. Getty images

Timu ya taifa ya soka ya Tanzania, yenye wachezaji wasiozidi miaka 17, wamepoteza mechi ya pili katika fainali ya kuwania taji la Afrika inayoendelea jijini Dar es Salaam.

Matangazo ya kibiashara

Tanzania ililemewa na Uganda kwa mabao 3-0 katika mechi ya pili, ya kundi A, kuwania taji hilo.

Mechi ya kwanza, Tanzania ilipoteza dhidi ya Nigeria kwa mabao 5-4.

Baada ya mechi ya pili, Tanzania ni ya mwisho katika kundi hilo bila ya alama, na hii inamaanisha kuwa haiwezi kufuzu katika hatua ya nusu fainali ili kwenda katika fainali ya Kombe la dunia nchini Brazil.

Nigeria nayo iliishinda Angola bao 1-0 na inaingoza kundi hilo kwa alama sita.

Leo Alhamisi, kuna mechi mbili za kundi B, Cameroon itamenyana na Morocco, huku Senegal ikimenyana na Guinea.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.