Pata taarifa kuu
AFRIKA-KOMBE LA SHIRIKISHO-SOKA

Etoile du Sahel yaiangusha Al Hilal kutinga nusu fainali kuwania taji la Shirikisho barani Afrika

Kombe la bara Africa
Kombe la bara Africa www.cafonline.com

Klabu ya Etoile du Sahel kutoka Tunisia na itachuana na Zamalek ya Misri, katika hatua ya nusu fainali, kuwania taji la Shirikisho barani Afrika.

Matangazo ya kibiashara

Hii ni baada ya ushindi wa mabao 5-2 baada ya mzunguko wa pili wa mechi ya robo fainali, iliyochezwa jijini Cairo siku ya Jumanne usiku.

Robo fainali ya kwanza, Etoile du Sahel ilipata ushindi wa mabao 3-1 na kuendeleza ushindi wa mabao 2-1 siku ya Jumanne.

Mchuano huu uliahirishwa wiki mbili zilizopita, kutokana na hali ya kisiasa nchini Sudan,  baada ya kuondolewa madarakani kwa rais Omar Al Bashir na hivyo Khartoum kutoonekana sehemu salama pa kuchezesa mechi hiyo ya marudiano.

Mechi ya kwanza ya mzunguko wa kwanza wa nusu fainali, itakuwa ni tarehe 28 mwezi Aprili huku mechi ya pili ikiwa ni tarehe tano mwezi Mei.

CS Sfaxien ya Tunisia na RS Berkane, nazo zitamenyana katika mechi nyingine ya nusu fainali.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.