Pata taarifa kuu
AFCON-CAF-SOKA-VIJANA

Guinea watinga hatua ya fainali, michuano ya vijana

Timu ya taifa ya Guinea ikimenyana na Nigeria katika nusu fainali ya mchezo wa soka kuwania ubingwa wa taji la Afrika kwa vijana wasiozidi miaka 17 jijini Dra es salaam Aprili 24 2019
Timu ya taifa ya Guinea ikimenyana na Nigeria katika nusu fainali ya mchezo wa soka kuwania ubingwa wa taji la Afrika kwa vijana wasiozidi miaka 17 jijini Dra es salaam Aprili 24 2019 RFI/Fredrick Nwaka

Time ya vijana ya Guinea Chini Ya Miaka 13 imefaulu Kucheza hatua ya fainali ya Michuano ya Afrika kwa vijana Chini ya Miaka 17 inayoendelea Jijini Dar es Salaam.

Matangazo ya kibiashara

Timu Hiyo Kutoka Afrika Magharibi Imepata ushindi Wa mikwaju ya penati 10-9 baada ya Timu Hizo Kutoka Sare ya Bila kufungana Katika dakika 90 za mchezo.

Kwa Matokeo hayo Guinea itachuana na mshindi baina ya Cameroon na Angola ambazo pia zimekuwa zikichuana jana.

Mwandishi Wa RFI Kiswahil, Fedrick Nwaka aliyeshuhudia Mchezo huo, anasema Nigeria Licha ya Kupewa Nafasi Kubwa ilishindwa Kufua dafu.

Licha ya Kupoteza mchezo huo Nigeria, Sanjari Na Angola, Guinea na Cameroon Zitawakilisha bara la Afrika Katika Fainali za vijana zitakazochezwa Baadaye Mwaka huu Nchini Brazil.

 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.