Pata taarifa kuu
AFCON 2019-TAIFA STARS-MISRI

Morocco:Taifa Stars imeimarika na iko tayari kushiriki fainali za Afrika

Kocha Msaidizi wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Hemed Morocco
Kocha Msaidizi wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Hemed Morocco Mtanzania

Kocha msaidizi wa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars, Hemed Morocco amesema kikosi cha timu ya Taifa, Taifa Stars kimeaimarika kabla ya kuanza kwa fainali za kombe la mataifa ya Afrika.

Matangazo ya kibiashara

Stars ilitoshana nguvu na Zimbabwe katika mechi ya mwisho ya kujiweka sawa kabla ya kuanza kwa fainali hizo Juni21.

"Tumecheza vizuri kulikoi mchezo uliopita na pia mchezo huu umetusaidia kubaini makosa yaliyojitokeza na tuna siku sita kabla ya kucheza mechi ya kwanza hivyo tutatumia muda huu kujiweka sawa,'amesema Morocco akinukuliwa na mtandao wa shirikisho la kandanda tanzania TFF.

Tanzania imepangwa kundi D na itafungua dimba kwa kuchuana na Senegal

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.