Pata taarifa kuu
KAGAME CUP-RWANDA-CECAFA

TP Mazembe kushiriki michuano ya Kombe la Kagame nchini Rwanda

Kikosi cha TP Mazembe, mabingwa mara tano wa taji la klabu bingwa Afrika
Kikosi cha TP Mazembe, mabingwa mara tano wa taji la klabu bingwa Afrika The New Times/Rwanda

Mabingwa wa soka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, TP Mazembe wamethibitisha kushiriki michuano ya Kombe la Kagame.

Matangazo ya kibiashara

Mashindano hayo yanayodhaminiwa na rais Paul Kagamae wa Rwanda yanatazamiwa kuanza Julai saba hadi 21.

Mazembe itaungana na timu nyingine kutoka DRC DC Motema Pembe na AS Vita Club na Zesco ya Zambia ambazo pia zimethibitisha kushiriki.

Simba na Yanga za Tanzania zilijiondoa kwenye mashindano hayo kewa sababu mbalimbali huku Azam FC ikiwa ni timu pekee kutoka Tanzania ambayo imesthibitisha kushiriki.

Hivi karibuni Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicholas Musonye alipuuzilia mbali kudorora kwa mashindano hayo baada ya timu za Tanzania kujiondoa.

 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.