Pata taarifa kuu
AFCON-BAFANA BAFANA-ANGOLA

Angola yafuta mechi ya kirafiki dhidi ya Afrika Kusini

Kikosi cha Timu ya Taifa ya Angola
Kikosi cha Timu ya Taifa ya Angola Egypt Today

Timu ya taifa ya Angola imefuta mchezo wa kirafiki dhidi ya Afrika kusini ulioapangwa kuchezwa leo nchini Misri.

Matangazo ya kibiashara

Mchezo huo ulipaswa kuwa sehemu ya maandalizi ya mwisho ya kikosi cha Angola maarufu kwa jina la Parancas Negras kabla ya kuanza kwa fainali za mataifa ya Afrika Ijumaa wiki hii.

Maofisa wa timu hiyo wanasema mchezo huo umefutwa baada ya kushindwa kupata uwanja wa kufanyia mazoezi tangu walipowasili nchini Misri kushiriki fainali hizo.

Wapinzani wa o Afrika kusini waliwasili mapema nchini Misri kwa ajili ya fainali hizo za 32 za mataifa ya Afrika ambazo kwa mara ya kwanza zitashirikisha nchi 24.

Angola imepangwa kundi E katika mashindano hayo ikiwa na timu za Tunisia, Mali na Mauritania

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.