Pata taarifa kuu
TAIFA STARS-TFF-AFCON

Mwantika arejeshwa kikosi cha Stars kuchukua nafasi ya Aggrey Moris

David Mwantika (wa pili kutoka kulia waliosimama) akiwa na wachezaji wenzake wa timu ya Taifa ya Tanzania
David Mwantika (wa pili kutoka kulia waliosimama) akiwa na wachezaji wenzake wa timu ya Taifa ya Tanzania Navva

Beki David Mwantika amerejeshwa kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars kilichopo nchini Misri kwa fainali za mataifa ya Afrika.

Matangazo ya kibiashara

Awali, Mwantika alikuwa miongoni mwa wachezaji saba walioachwa na Kocha Emanuel Amunike baada ya kambi ya maandalizi ya wiki moja nchini Misri.

Ripoti zan kurejeshwa kikosini kwa mlinzi huyo zimechapishwa na mtandao wa gazeti la michezo nchini Tanzania la Mwanaspoti na zinakuja baada ya beki Aggrey Morris kupata jeraha la mguu katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Zimbabwe.

Tayari mchezaji huyo yu angani akielekea nchini Misri kwa mujibu wa duru za taarifa ndani ya mamlaka za soka la Tanzania, TFF.

Tanzania nitaanza kampeni ya kushiriki fainali hizo Juni 23 kwa kuchuana na Senegal katika Uwanja wa Michezo wa kimataifa wa cairo.

 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.