Pata taarifa kuu

Burundi, Taifa Stars zaahidiwa kitita cha fedha kuelekea Afcon

Mataifa yatakayoshiriki fainali za Afrika zinazoanza kesho nchini Misri
Mataifa yatakayoshiriki fainali za Afrika zinazoanza kesho nchini Misri Bien Sports

Serikali ya Tanzania leo imefanya harambee ya kuichangia timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars ambayo iko nchini Misri kushiriki fainali za Afrika.

Matangazo ya kibiashara

Hafla hiyo imefanyika katika hotel ya Serena na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali ambapo mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Tanzania, samia Suluhu Hassan amenunua jezi ya timu hiyo kwa shil;ingi milioni tano huku wa ziri wa Habari Harrison Mwakyembe akinunua kwa shilingi milioni moja.

Mamilioni ya fedha yamechangwa na kampuni na taasisi mbalimbali huku mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akiahidi kutoka eneo la uwanja wa hekari 15 kwa shirikisho la soka Tanzaniam TFF kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha soka.

Makamu wa rais amewataka watanzania kuisapoti kwa hali na mali timu hiyo wakati wote itakapokuwa ikishiriki.

Ripoti kutoka Burundi zinasema Shirikisho la Soka limeahidi kutoa Faranga za Burundi milioni 150 karibu dola 7000 ikiwa Burundi itaishinda Nigeria katika mchezo wa Afcon.

 

 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.