Pata taarifa kuu
AFCON-TANZANIA-SENEGAl

Kenya na Tanzania zaingia uwanjani kusaka ushindi katika fainali za Afcon

Wachezaji wa Taifa Stars David Mwantika na John Bocco wakiingia uwanjani kwa mazoezi ya mwisho kabla ya kuchuana na Senegal leo Jumapili
Wachezaji wa Taifa Stars David Mwantika na John Bocco wakiingia uwanjani kwa mazoezi ya mwisho kabla ya kuchuana na Senegal leo Jumapili TFF/Twitter

Timu za Taifa za Kenya na Tanzania zinashuka uwanjani leo kuchuana na Algeria na Senegal katika mfululizo wa fainali za Afrika zinazofanyika nchini Misri.

Matangazo ya kibiashara

Mataifa hayo jirani yamepangwa kundi moja la C sambamba na Senegal na Algeria, timu zinazotajwa kuwa miamba ya soka barani Afrika.

Katika Uwanja wa Juni 30 Taifa Stars inayonolewa na Mnigeria Emanuel Amunike itachuana na Senegal majira ya saa mbili usiku kwa saa za Afrika mashariki na baadaye Kenya itachuana na Algeria.

Mashabiki na wachambuzi wa kandanda nchini Tanzania wamemiminika mtandaoni wakiitakia kheri Taifa Stars inayorejea katika fainali za Afrika baada ya karibu miaka 40.

Nayo Kenya inarejea tena katika mashindano hayo makubwa ya kanda barani Afrika baada ya miaka 15.

Kocha wa Taifa Stars Emanuel Amunike amesema licha ya kucheza na timu bora barani Afrika, Taifa Stars iko tayari kwa mchezo huo huku akiahidi wachezaji wake kujitolea uwanjani.

Jana Burundi licha ya kujitutumua muda mwingi wa mchezo ilishindwa kwa bao 1-0 dhidi ya Nigeria huku Madagascar na Guinea zikitoshana nguvu kwa kufungana mabao 2-2

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.