Pata taarifa kuu
TANZANIA-TAIFA STARS-CHAN2020-CAMEROON

Makumi wailaki Taifa Stars baada ya kufuzu fainali za CHAN

Kikosi cha Taifa stars kilichochuana na Sudan jana Oktoba 19 mwaka 2019 Mjini Khartoum
Kikosi cha Taifa stars kilichochuana na Sudan jana Oktoba 19 mwaka 2019 Mjini Khartoum Instagram/TFF

Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars imerejea jijini Dar es Salaam siku moja baada ya kufuzu kushiriki fainali za Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani CHAN. 

Matangazo ya kibiashara

Stars imekuwa timu ya kwanza kukata tiketi ya kushiriki mashindano hayo baada ya kuishinda Sudan mabao 2-1 katika mchezo uliochezwa Mjini Khartoum, Stars ikifuzu kwa uwiano mzuri wa mabao ya ugenini.

Fainali za Chan zinazoshirikisha timu 16 zitafanyika mwaka 2020 nchini Cameroon.

Katika mchezo wa kwanza uliochezwa mjini Dar es Salaam, Tanzania ilishindwa kwa bao 1-0.

Mabao yaliyoipeleka Tanzania katika fainali hizo yalifungwa na mlinzi Erasto Nyoni na mshambuliaji Ditram Nchimbi ambaye alikuwa akicheza mchezo wa kwanza wa timu ya Taifa.

Kocha msaidizi wa Taifa Stars, Suleiman Matola amesema haikuwa kazi rahisi kupata tiketi hiyo.

“Tumepambana na Kenya na Sudan zote zilikuwa mechi ngumu, kwa sasa tumerudi na tutaweka mikakati ya kiufundi kabla ya mashindano,”amesema Matola mchezaji wa zamani wa taifa Stars na klabu ya Simba ya Tanzania na Supersport ya Afrika Kusini.

Tanzania inafuzu kwa mara ya pili kushiriki fainali hizo, mara ya kwanza ilishiriki fainali hizo mwaka 2009 zilizofanyika nchini Ivory Coast.

Mwandishi wetu Fredrick Nwaka alifika auwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere ambapo raia aliozungumza nao wamesema wanamatumaini Tanzania itaendelea kunawiri katika mchezo wa kandanda.

Mashabiki wa soka Tanzania waliojitokeza kuilaki Taifa Stars Mjini Dar es Salaam 19 Oktoba 2019
Mashabiki wa soka Tanzania waliojitokeza kuilaki Taifa Stars Mjini Dar es Salaam 19 Oktoba 2019 RFI/Fredrick Nwaka

stars 1

Mataifa mengine ya Afrika mashariki na kati yanayoweza kukata tiketi mwishoni mwa juma hili ni Rwanda, Uganda na DRC

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.