Pata taarifa kuu
FIBA-TBF-KIKAPU-KLABU BINGWA AFRIKA

JKT yaduwazwa na Patriots, klabu bingwa ya kikapu Afrika

Oilers ilipopambana na timu kutoka Rwanda katika Uwanja wa ndani wa Taifa Jijini Dar es Salaam Oktoba 5, 2018
Oilers ilipopambana na timu kutoka Rwanda katika Uwanja wa ndani wa Taifa Jijini Dar es Salaam Oktoba 5, 2018 RFI Kiswahili/Fredrick Nwaka

Michuano ya klabu bingwa Afrika kwa mpira wa kikapu inafikia tamati nchini Tanzania leo huku wawakilishi wa tanzania JKT wakishindwa kufua dafu.

Matangazo ya kibiashara

Jana, JKT ilishindwa na Patriots ya Rwanda kwa vikapu 79 kwa 65, ukiwa ni mchezo wa pili kupoteza.

Michuano hiyo ya Kundi D inachezwa nchini Tanzania na kushirikisha timu za City Oilers ya Uganda, Dynamos ya Burundi, Patriots ya Rwanda na JKT ya Tanzania. Timu ya Breva Heart ya Malawi haikufika kutokana na sababu za ukata.

Timu mbili zitakzofanya vyema zitaungana na timu nyingine sita kucheza hatua ya nane bora ya michuano hiyo ambayo inachezwa kikanda.

Mechi za mwisho leo ni baina ya Patriots ya Rwanda dhidi ya City Oilers ya uganda na JKT ya Tanzania itachuana na Dinamo ya Burundi.

Hata hivyo kocha wa Patriots Henry Mwinuka amesema miundombinu ya uwanja wa ndani wa taifa ina changamoto kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.