Pata taarifa kuu
SOKA-MISRI-AFRIKA-VIJANA

Misri yafuzu hatua mwondoano michuano ya Vijana barani Afrika

Timu ya taifa ya Misri yenye wachezaji wenye chini ya umri wa miaka 23
Timu ya taifa ya Misri yenye wachezaji wenye chini ya umri wa miaka 23 REUTERS/Amr Abdallah Dalsh

Wenyeji Misri wanacheza mechi ya mwisho dhidi ya Cameroon, ikiwa ni hatua ya makundi, kuwania taji la vijana barani Afrika katika mchezo wa soka, kwa wachezaji waozidi miaka 23. 

Matangazo ya kibiashara

Mechi mbili zilizopita, Misri imeshinda michuano yote, na tayari imefuzu katika hatua ya mwondoano.

Mali ambao tayari wameondolewa katika michuano hii, baada ya kufungwa mechi mbili zilizopita, wanamaliza kazi na Ghana.

Michuano hii pia inatumiwa kufuzu kushiriki katika michuano ya Olimpiki mwaka ujao jijini Tokyo nchini Japan.

Katika michuano ya kundi B, mechi za kundi hilo yanamalizika siku ya Ijumaa. Nigeria, itachuana na Afrika Kusini, huku Ivory Coast ikimenyana na Zambia.

Afrika Kusini inaongoza kundi hilo kwa alama 4, huku Ivory Coast na Nigeria zikiwa na alama tatu.

Zambia ambayo pia inaweza kufuzu, ina alama moja.

 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.