Pata taarifa kuu
CECAFA-KENYA-TANZANIA-UGANDA-BURUNDI-RWANDA

Michuano ya Cecafa:Kenya ilinuia kutwaa taji

Wachezaji wa timu ya wanawake ya Kenya, Harambee Starlets wakishangilia baada ya kutwaa ubingwa wa Cecafa kwa kuishinda Tanzania Bara kwa mabao 2-0 katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam, Tanzania 25 Novemba 2019
Wachezaji wa timu ya wanawake ya Kenya, Harambee Starlets wakishangilia baada ya kutwaa ubingwa wa Cecafa kwa kuishinda Tanzania Bara kwa mabao 2-0 katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam, Tanzania 25 Novemba 2019 RFI/Fredrick Nwaka

Michuano ya Cecafa kwa wanawake imemalizika jana Novemba 25, 2019 nchini Tanzania na kushuhudia Kenya ikinyakua taji hilo kwa kuishinda Tanzania Bara kwa mabao 2-0.

Matangazo ya kibiashara

Ni mashindano makubwa kwa wanawake katika kanda hiina kwa hakika yanatoa taswira ya wapi soka la wanawake lilipo na linapokwenda.

Tanzania waliingia katika michuano hiyo kama mabingwa watetezi mtawalia.

Mwandishi wa RFI Kiswahili, Fredrick Nwaka ameshuhudia michuano hiyo na ameangazia namna mataifa manae yalivyoshiriki michuano hiyo na ushindani ulivyoonekana.

Yalikuwa mashindano ya timu tatu.

Tangu kuanza kwa michuano hiyo Kenya, Uganda na Tanzania Bara ndizo timu zilizoonekana mapema kujiandaa kikamilifu. Tanzania Bara wakiingia kama mabingwa watetezi walikuwa kambini kwa mwezi mmoja huku Kenya wakitoka kushiriki michuano ya kusaka tiketi ya kushiriki michuano ya Olimpiki. Tangu awali katika hatua ya makundi mataifa haya matatu yalionyesha wazi kuwa yako sawa kwa kupata ushindi mnono katika mechi nza hatua ya makundi.

Wachezaji wa Kenya na Tanzania Bara kabla ya kuanza kwa mchezo wa fainali ya kombe la Cecafa katika Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam. Novemba 25, 2019
Wachezaji wa Kenya na Tanzania Bara kabla ya kuanza kwa mchezo wa fainali ya kombe la Cecafa katika Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam. Novemba 25, 2019 RFI/Fredrick Nwaka

 

Ugeni wa Djibout na Sudan Kusini

Djibout na nchi changa ya Sudan Kusini zimeshiriki michuano hiyo kwa mara ya kwanza na hazikufanya vyema katika hatua ya makundi, Sudan kusini ikishinda mchezo mmoja pekee dhidi ya Zanzibar.

Kocha wa Sudan Kusini, Simon James aliimbia RFI Kiswahili kuwa timu yake imekuja kujifunza na haikutarajia kutoa ushindani tofauti na timu zenye uzoefu.

Zanzibar wakosa uzoefu

Timu ya Taifa ya Zanzibar imeshiriki mashinda hayo mara kadhaa lakini bado haijafanikiwa kuopenya na kufuzu kutoka hatua ya makundi. Musonye anasema kupitia mradi wa fowartd unaotekelezwa na Fifa Cecafa inaamini utasaidia baadhi ya maeneo kama Zanzibar kuboresha ligi za wanawake na vijana. Zanzibar walipoteza mechi zote za hatua ya makundi dhidi ya Tanznaia Baram Sudani Kusini na Burundi.

Mashabiki waliyabeba mashindano

Ni dhahiri mashabiki wa soka nchini Tanzania walikuwa chachu ya michuano hiyo, kwa kujitokeza kwa wingi tangu mwanzo wa michuano hiyo. Katika kutambua hilo Musonye ameweka wazi kuwa Cecafa inajivua Tanzania kuwa mwenyeji wa mashindano hayo na kutaka nchi nyingine wanachama kuiga mfano wa Tanzania. Tanzania inasalia kuwa taifa muhimu katika ukanda wa Cecafa hususani linapokuja suala la kuandaa mashindano mbalimbali na msisimko wake.

Viwanja vya nyasi bandia ni changamoto

Ni dhahiri stamina ya wanaume na wanawake ni tofauti, uwanja wa Azam Complex uliotumika katika mashindano hayo umejengwa kwa nyasi bandia (artificial grass). Kila baada ya muda w aamuzi walilazimika kusimamisha mchezo ili kutoa fursa kwa wachezaji kunywa maji. Halikadhalika wachezaji wengi walionekana kuzidiwa kuhimili nyasi bandia na wengine kuumia.

Kenya ilijiandaa kushinda taji

Ni wazi Kenya ilinuia kutwaa ubingwa huu. Naibu rais wa FKF Doris Petra ameiambia RFI Kiswahili kuwa vijana waliotwaa taji waliandaliwa kwa kipindi kisichozidi mwaka mmoja kutoka shule mbalimbali za msingi na sekondari. Ni wazi mkakati huu ukitekelezwa na mataifa ya Cecafa huenda tukashuhudia azima ya ukanda wa Cecafa kutoa timu itakayoshiriki kombe la dunia miaka kadhaa ijayo.

Kukosekana kwa baadhi ya timu.

Rwanda, Sudan, Eritrea na Somalia hazikushiriki michuano hiyo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ukosefu wa fedha. Ni wazi msisimuko wa mashindano unapungua kwa kukosekana kwa mataifa haya. Mbele ya safari kuna haja kwa cecafa kutafuta wadhamini watakaojitokez akugharamia maradhi na usafiri kwa nchi shiriki.

Pongezi kwa Cecafa

Uongozi wa Cecafa kupitia sekretarieti yake inayoongozwa na katibu Mkuu Nicholas Musonye unastahili pongezi kwa uthubutu wake. Mashindanio haya ya wanawake yalipoteza machoni pa mashabiki wa soka lakini kwa sasa kila mtu kwenye kanda hii anazungumza mashindano haya na umuhimu wake katika kukuza mchezo wa soka. Kuna haja ya kuhakikisha mashindano haya yanaendelea kusimamiwa kikamilifu ili yawe endelevu.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.