Pata taarifa kuu
LIBERIA-WEAH-SIASA

George Weah kugombea kiti cha urais 2017

Mpinzani na aliyekuwa nyota wa kimataifa wa soka George Weah wakati wa mkutano wa kampeni. Monrovia, Novemba 20, 2014.
Mpinzani na aliyekuwa nyota wa kimataifa wa soka George Weah wakati wa mkutano wa kampeni. Monrovia, Novemba 20, 2014. AFP PHOTO / ZOOM DOSSO

Aliyekuwa mchezaji wa soka nchini Liberia George Weah ametangaza rasmi kuwania urais nchini humo mwezi Oktoba mwaka ujao.

Matangazo ya kibiashara

Mwaka 2005 aliwania kwa mara ya kwanza lakini hakufanikiwa kupata ushindi, lakini pia mwaka 2011 alijiondoa katka kinyang'anyiro cha kuwania Umakamu wa rais.

Weah ambaye anaongoza chama cha Congress for Democratic Change, anasema lengo lake ni kuleta mabadiliko na uongozi mpya katika nchi yake.

Anasalia kuwa katika vitabu vya historia kwa kuwa mchezaji wa kipekee kutoka barani Afrika aliyewahi kuwa mchezaji bora wa mchezo wa soka duniani.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.