Pata taarifa kuu
BOLIVIA-SIASA

Rais wa Bolivia kuwania muhula wa nne, raia wamiminika mitaani

Rais wa Bolivia Evo Morales, Tiquipaya, Bolivia Novemba 28, 2017.
Rais wa Bolivia Evo Morales, Tiquipaya, Bolivia Novemba 28, 2017. Enzo De Luca/Courtesy of Bolivian Presidency/Handout via REUTERS

Rais wa Bolivia Evo Morals ametangaza kuwa atawania urais kwa muhula wa nne mwaka 2019. Hatua hii imezua maandamano makubwa pindi tu Mahakama ya Kikatiba kuondoa mihula ya rais kuongoza nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Mahakama ya Katiba ya Bolivia siku ya Jumanne ilimruhusu rais Evo Morales kuwania muhula mwingine mwaka 2019, ingawa wananchi wa taifa hilo walimkatalia katika kura ya maoni iliyopigwa mnamo mwezi Februari 2016.

Morales amewaambia wafuasi wake kuwa pia amepata shinikizo kutoka kwa wanasiasa wa upinzani nchini Marekani kuwa, awanie tena.

Evo Morales, mwenye umri wa miaka 58, alishindwa katika jaribio lake la kurekebisha katiba mnamo mwezi Februari 2016 ili kumruhusu kuwania muhula wa nne (2020-2025) baada ya wananchi wa Bolivia kumkatalia katika kura ya maoni ambapo kura ya "Hapana" ilishinda. Chama chake cha MAS kinatafuta kwa njia zote ili kuzuia kura hiyo ya "Hapana".

Katika kutetea uamuzi wake, Mahakama ya Katiba ilibaini kwamba haki ya kuwania kwa uhuru wadhifa huo ilikuwa kubwa kuliko kikomo kilichowekwa na Katiba.

Kwa mujibu wa Bw Morales, kura ya "hapana" ilipata ushindi mdogo wakati wa kura ya maoni ya mwaka 2016 kwa sababu ya "uongo" uliofichuliwa muda mfupi kabla ya kura.

Kushindwa huko kwa kisiasa kuliwastaajabisha wengi kwa rais wa Bolivia, nchi ya Amerika Kusini, alietawala kwa muda mrefu tangu mwaka 2006.

Evo Morales, anadai kuwa ndiye rais wa kwanza kuongoza Bolivia kwa muda mrefu.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.