Pata taarifa kuu
DRC-UDPS-SIASA

Chama cha UDPS chaendelea kupoteza nguvu DRC

Waziri Mkuu wa DRC, Bruno Tshibala.
Waziri Mkuu wa DRC, Bruno Tshibala. JUNIOR KANNAH / AFP

Chama Kikuu cha upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, UDPS kimesema kinapanga kwenda katika Mahakama ya Kikatiba, kuwasilisha kesi ya kumtaka Waziri Mkuu Bruno Tshibala ajiuzulu.

Matangazo ya kibiashara

UDPS inasema inapanga kuchukua hatua hii, baada ya Tshibala kuitisha kikao ambao wanasema hawakitambui na akachaguliwa kama kiongozi wa chama hicho kinachoonekana kugawanyika.

Chama hicho kinasema Tshibala amevunja katiba kwa mujibu wa kifungo cha 97.

Mkutano huo umekigawa chama hicho ambacho kilikuwa kinaongozwa kwa muda mrefu na Etienne Tshisekedi aliyefariki dunia mapema mwaka huu.

Tshibala amesema atafanya kila kilicho ndani ya uwezo wake kurejea katika Ofisi ya chama hicho.

Mapema wiki hii Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Reuben Mikindo, alisema hawamtambui Tshibala kama mwanachama wa chama chao baada ya kumfukuza.

Mvutano umeshika kasi katika chama hicho cha upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuwania mrithi wa mwenyekiti wa chama hicho Etienne Tshisekedi aliefariki miezi kadhaa iliyopita..

mwishoni mwa juma lililopita Bruno Tshibala alisema chama cha UDPS sio taasisi ya jadi ambayo mtoto anamrithi baba yake.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.