Pata taarifa kuu
VENEZUELA-SIASA

Muungano wa upinzani wapigwa marufuku kushiriki uchaguzi Venezuela

Andres Velasquez na wanachama wengine wa MUD, katika mkutano na waandishi wa habari, Caracas mnamo Januari 24, 2018.
Andres Velasquez na wanachama wengine wa MUD, katika mkutano na waandishi wa habari, Caracas mnamo Januari 24, 2018. REUTERS/Adriana Loureiro

Mvutano kati ya serikali ya Venezuela na upinzani unaendelea kushuhudiwa. Baada ya kutangaza siku ya Jumatatu, uchaguzi wa rais kufanyika kabla ya mwisho wa mwezi Aprili, serikali, kupitia Mahakama Kuu, imeamua kupiga marufuku muungano wa upinzani kujiandikisha kama chama cha siasa.

Matangazo ya kibiashara

Mbinu ya kisiasa inayolenga kuugawanya muungano huo, na mbinu hii itapelekea rais wa sasa Nicolas Maduro kushinda uchaguzi.

Muungano wa upinzani MUD alisusia uchaguzi wa majimbo wa hivi karibuni, na kwa sasa unaonekana unaendelea kuminywa na serikali ya Venezuela. Uamuzi huo wa Mahakama Kuu, ambao unalenga kufuta muungano huo wa upinzani MUD (Democratic Unity Roundtable) ni aina ya pigo kwa vyama vya siasa vinavyoonekana zaidi kugawanyika katika siku za hivi karibuni.

Kwa sasa muungano huo unaonekana hauna kiongozi halisi, kwa sababu viongoizi wawili ambao ni vigogo wa MUD sasa hawacharuki kutokana na maamuzi ya mahakama. Henrique Capriles, kiongozi wa chama cha Primero Justicia, hana haki ya kugombea katika nafasi yoyote, ambaye alikosea kupata ushindi dhidi ya mrithi wa Hugo Chavez, Nicolas Maduro, katika uchaguzi wa mwaka 2013. Na Leopoldo Lopez, ambaye amehukumiwa zaidi ya miaka 13 jela, yuko chini kifungo cha nyumbani.

Pamoja na mbinu hii, utawala uliopo madarakani nchini Venezuela unapunguza kwa kiasi kikubwa uwezekano wa ushindi wa mgombea wa upinzani. Maana kwa kufanya hivyo, serikali inataka kuepo na wagombea wengi kutoka vyama vya upinzani na kupunguza uwezekano wa ushindi wa mgombea kutoka vyama hivyo vinavyounda muungano huo wa MUD.

Wataalamu wengi bila shaka na upinzani, ambao unaweza kususia mazungumzo yaliyopangwa kufanyika Januari 28 na 29 katika Jamhuri ya Dominika.

Ufaransa yatoa msimamo wake baada ya uamuzi wa Mahakama Kuu

Kwa majibu wa wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa (Quai d'Orsay), kupigwa marufuku kwa MUD kushiriki uchaguzi ujao wa rais nchini Venezuela ni "kukiuka haki ya msingi" ya uchaguzi. "Mamlaka ya Venezuela kwa mara nyingine imekiukwa haki ya uchaguzi huo, baada ya kubadilisha kalenda ya uchaguzi bila kushauriana na upinzani," amesema msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni ya Ufaransa.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.