Pata taarifa kuu
NIGERIA-UINGEREZA-UCHUMI

Uingereza yatakiwa kurejesha mali kutoka Afrika

Shirika la Ulaya linaloshughulikia dawa lenye makao yake makuu London, mji mkuu wa Uingereza ambayo inashtumiwa kuwa kinara kwa kuwa na mali nyingi zilizoibiwa kutoka Afrika.
Shirika la Ulaya linaloshughulikia dawa lenye makao yake makuu London, mji mkuu wa Uingereza ambayo inashtumiwa kuwa kinara kwa kuwa na mali nyingi zilizoibiwa kutoka Afrika. Daniel LEAL-OLIVAS / AFP

Nchi ya Nigeria na mataifa mengine ambayo yalitawaliwa na Uingereza yameanzisha kampeni ya kutaka kurejeshwa kwa mali ambazo ziliibiwa ikiwemo mabilioni ya dola yanayohifadhiwa kwenye akaunti za nje.

Matangazo ya kibiashara

Haya yanajiri wakati huu ambapo nyakati fulani aliyekuwa waziri mkuu wa Uingereza David Cameroon alidai bara la Afrika limekithiri kwa vitendo vya rushwa lakini takwimu zinaonesha kuwa nchi ya Uingereza ni kinara kwa kuwa na mali nyingi zilizoibiwa kutoka Afrika.

Katika mkutano uliofanyika mwishoni mwa juma jijini Abuja Nigeria na kuwakutanisha wakuu wa taasisi za kupambana na rushwa barani Afrika, walikubaliana kuanzisha mchakato utakaofanikisha kurejeshwa kwa mali hizo.

Wakuu hao wametoa wito wa viongozi wa bara la afrika kuunganisha nguvu kupambana na vitendo vya rushwa na kuongeza uwazi katika serikali zao ikiwa ni pamoja na kubaini na kuzirejesha mali zilizoibwa.

Katibu mkuu wa jumuiya ya madola Patricia Scotland amesema bara la Afrika linapoteza mabilioni ya dola za Marekani kila mwaka kutokana na rushwa, wizi na utakatishaji fedha.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.