Pata taarifa kuu
MISRI-SIASA

Abdel Fattah al-Sisi kuapishwa Juni 2 kama rais wa Misri

Watu wakishangilia bango kubwa lenye picha ya Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi mbele ya Mahakama ya Juu, katikati mwa mji wa Cairo.
Watu wakishangilia bango kubwa lenye picha ya Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi mbele ya Mahakama ya Juu, katikati mwa mji wa Cairo. REUTERS/Amr Abdallah Dalsh

Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi ataapishwa tarehe mbili mwezi ujao kuongoza nchi hiyo kwa muhula wa pili. Hii itakuja baada ya kushinda Uchaguzi wa urais uliofanyika mwezi Machi kwa kupata ushindi wa asilimia 97.

Matangazo ya kibiashara

Kwa matazamo wa watu wanaomuunga mkono rais Abdel Fattah Al-Sisi ni wazi kwamba Misri inasonga mbele kwa sababu nchi yao inaongozwa na mtekelezaji na siyo na mwanasiasa. Hivyo ndivyo al-Sisi anavyoeleweka kwa wafuasi wake: Hotuba fupi lakini matendo ni marefu na yeye mwenyewe anathibitisha kwa kueleza na hapa namnukuu:-

Rais al-Sisi, mara nyingi anasema: ‘'Mimi si mwanasiasa, anayehutubia tu. Tunaijenga nchi yetu siyo kwa maneno. Mola anajua jinsi Misri ilivyorejea tena!”.

Rais al-Sisi anatokea kwenye nasaba ya chini. Alimaliza kazi ya jeshini akiwa na cheo cha Jenerali. Katika mchakato wa kumpindua rais wa hapo awali Mohammed Morsi mnamo mwaka 2012 al-Sisi ndiye aliekuwa anaongoza operesheni hiyo .Mnamo mwaka wa 2014 aligombea urais  na kushinda kwa kupata asilimia karibu 97 ya kura. Aliungwa mkono kwa kias kikubwa na wanawake , na ndiyo sababu amesema akina mama wanastahili kuheshimiwa.

Wapo wanawake sita katika serikali ya Misri idadi hiyo haina kifani katika historia ya nchi hiyo. Al-Sisi ni muumini wa dini sawa na Wamisri wengi. Mara kwa mara anainukulu Qur'ani Tukufu na bila ya kujali anawakabili viongozi wa dini kwa kutoa mwito wa kuleta usasa katika uislamu.

Mnamo mwaka wa 2015 rais al-Sisi alihudhuria misa ya Krismas ya kanisa la Koptik. Hakuna rais mwengine yeyote wa Misri aliewahi kuchukua hatua kama hiyo. Katika nchi za magharibi, ikiwa pamoja na nchini Ujerumani, al-Sisi anazingatiwa kuwa nguzo ya utengemavu. Imani hiyo ilimpa mwanya wa kutumia mkono wa chuma katika muhula wake wa kwanza wa urais. Aliwahi kumkaripia mbunge aliyemwomba kuahirisha uamuzi wa kupandisha bei ya nishati. Alimuuliza mbunge huyo iwapo alikijua alichokuwa anakizungmzia bungeni.

Katika juhudi zakuukabili mgogoro wa uchumi mnamo mwaka wa 2011 kiongozi huyo wa Misri alichelewa kuchukua hatua za kuleta mageuzi alizotakiwa kuchukua na Shirika la fedha la kimataifa IMF. Masharti yalitolewa na IMF yalisababisha bei kupanda lakini yameufanya uchumi wa Misri uwe na ufanisi.

Kwa mujibu wa katiba ya sasa ya nchini Misri  al-Sisi hataruhusiwa kugombea muhula wa tatu wa urais.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.