Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA-UCHUMI

Bei ya unga wa ngano yapanda 25% Kinshasa

Mkate ni chakula kinachotumiwa na wakaazi wengi wa mjini Kinshasa.
Mkate ni chakula kinachotumiwa na wakaazi wengi wa mjini Kinshasa. © AFP

Bei ya unga wa ngano imepanda 25% mjini Kinshasa nchini DRC baada ya kiwanda cha kutengeneza unga huo kufungwa mwishoni mwa mwezi Agosti "kwa sababu ya ajali", wamiliki wa maduka ya vyakula katika mji huo wamesema.

Matangazo ya kibiashara

Bei ya mfuko wa unga wa ngano wa kilogramu 45 umepanda hadi dola 7 kutoka dola 28 hadi dola 35 katika maduka ya jumla huko Kinshasa, kwa mujibu wa wauzaji wa mkate ambao wana hofu ya kupanda kwa bei ya chakula hicho kikuu kinachotumiwa na karibu wakaazi wa Kinshasa milioni kumi.

Ongezeko hili linakuja "baada ya kufungwa kwa kiwanda cha kutengeneza unga wa ngano cha FAB-Congo, kwa sababu ya ajali, moja ya viwanda vitatu vikuu vinavyotengeneza unga wa ngano mjini Kinshasa ," Mbunge Toussaint Alonga ameliambia shirika la Habari la AFP.

Mwishoni mwa mwezi Agosti, mitambo ya FAB-Congo ilianguka na kudondokea hospitali jirani, na kuua watu wanne.

Serikali imeendelea kusema kuwa bei ya mkate haijapanda. Mkate unauzwa faranga ya Congo 200 kwa hofu ya kuhatarisha usalama wa taifa.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.